May 22, 2013

JISIKIE VIZURI NA JIONE MTANASHATI


 
kujisikia vyema kuhusu mwili wako ni jambo la msingi sana katika kujiona wewe ni bora.... ukijisikia vyema juu ya mwili wako lazima utautunza na kuwa mtanashati na pia na kujisikia vyema muda mwingi.

kujisikia vizuri kuhusu mwili wako hakuhitaji wewe kuwa mwembamba, unahitajika kuwa fit na mwenye afya njema na kujisikia vyema. vyovyote ulivyo wewe ni mzuri tatizo ni huo tunajisahau kujali afya zetu matokeo yake tunaangukia kwenye kula vyakula ambavyo vinatupelekea kwenye unene uliopitiliza ambao si mzuri kiafya.

hivyo basi vyovyote ulivyo jisikie vyema.... hakikisha unakula chakula bora na kufanya mazoezi mara kwa mara.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...