....mauaji au game....semeni nyie mie hata maelezo nimekosa
Dec 21, 2010
Eto'o Mchezaji Bora wa Afrika
kwa kushinda tuzo hiyo mara nne Eto'o amewazidi wakongwe wa soka ambao walishawahi kushinda tuzo hiyo mara tatu wote wawili ambao ni Abedi Pele na George Weah.
Dec 20, 2010
serengeti boys yachapwa 1-0
Kocha wa Tanzania Jamhuri Kiwhelu amesema kuwa Timu yake ilicheza vizuri licha ya kufungwa bao hilo la penati.
Dec 17, 2010
Kobe na kumbukumbu za alikotoka..
Kocha Downer bado anafundisha timu ya shule ile ile ambayo alisoma Kobe inayojulikana kwa jina la Merion High School iliyopo Philadelphia.
Kwa kuonyesha shukurani zake kwa kocha wake huyo Kobe anatarajia kutembelea shule hiyo Alhamisi ijayo kuhudhuria sherehe kwenye gym ambayo wameipa jina lake. Kobe ameahidi kiasi cha $411,000 kwa ajili ya maendeleo ya elimu na michezo katika shule hiyo.
Dec 16, 2010
Mhhhhhhhhh...
Forlan apewa Adidas Golden Ball
Mshambuliaji Diego Forlan wa Uruguay amekabidhiwa rasmi tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Dunia inayoitwa Adidas Golden Ball baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora katika Fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika nchini Afrika Kusini.
Forlan alikabidhiwa tuzo hiyo na mchezaji mkongwe wa soka Franz Beckenbauer katika sherehe iliyofanyika nchini Ujerumani.
Dec 15, 2010
Dec 14, 2010
Dec 8, 2010
HII KALI....
Ingekuwa poa kweli kama magorofa kama haya yangejengwa karibu na Neshno stadium, tungekuwa hatuna tabu ya kulipa miviingilio....
Dec 7, 2010
JISIKIE VIZURI JINSI ULIVYO........
Kila mtu, mnene au mwembamba alishawahi kwa kipindi fulani kujifeel negatively kuhusu miili yao. Njia rahisi ya kujisikia vizuri kuhusu mwili wako ni kuhakikisha kwamba unakuwa mtanashati kwa kiwango cha juu unachoweza. sio unatoka wako umesahau kunawa uso, umesahau kupiga pasi nk.
Mambo ya kuzingatia:
1. Unatakiwa kujiambia kila siku unapojitazama kwenye kioo kuwa hicho unachoona ni kizuri na utaendelea kukiboresha. hakikisha umependeza, unanukia vizuri kama ni mwanaume kaka una bashasha na bibie full mashamsham hapo toka elekea kwenye shughuli zako hakika utakuwa unajisikia vizuri.
2. Rome haikujengwa kwa siku moja!! kama una kilo 101 ukipunguza nusu jisifie ona hayo ni mafanikio sio una kilo 101 unataka ulale uamke ufanane na shoga yako mwenye kilo 51. jipongeze kwa kila hatua ndogo unayo piga na usikate tamaa.
3. Hakikisha unakula mlo sahihi unaoendana na matakwa yako, kama unataka kupunguza uzito basi hakikisha unakula mlo sahihi.
4. Kujiremba.
-Hakikisha unapotoka kwako asubuhi umejiremba, usoni namaanisha.
-Hakikisha nyele zako ziko vizuri, tafuta mionekano mipya ya nywele, jaribu style mpya za nyele sio unatutokea kwako na mibutu au minywele imeota kama saluni huzioni vile.
-Vaa nguo inayoendena na rangi yako na mwili wako sio ujipige mimake-up ya ukweli,nywele unaeleweka halafu nguo unatuvalia
mazwazwa...piga pamba unayokufanya utoke.
-Vaa viatu vinavyokufanya uonekane smart.
Dec 6, 2010
PAMOJA TENA......
kwanza niwaombe radhi wadau wote wa blog hii kwa kutoweka kwa muda mrefu lakini yote hiyo ni kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu.
sasa tupo pamoja tena
nawapenda.
sasa tupo pamoja tena
nawapenda.
Subscribe to:
Posts (Atom)