Nov 26, 2012

FAIDA ZA SABUNI YA LIWA (sandalwood soap)

historia ya matumizi ya mti wa liwa katika kuboresha na kuipa afya ngozi inaanzia zamani sana katika nchi za Egypt, China na India...kwa miaka mingi sana inajulikana kwa uwezo wake wa kuboresha ngozi na kuipa afya...liwa imeweza kutengenezwa katika mionekano mbalimbali kama mafuta, maji ya liwa na sabuni....
 
kwa wale ambao hawajawahi kuuona mti wa liwa ndio huu unakua mkubwa kabisaaaa
 

tukizungumzia sabuni ya liwa ambayo ina faida nyingi katika ngozi zetu ambazo ni:
i)  kulainisha ngozi
ii) kufanya ngozi iwe nyororo na yenye afya
iii)pia inasaidia kuondoa muwasho, harara, vipele na harufu mbaya

sabuni ya liwa


jamani hizi sabuni ni nzuri sana na zina saidia sana kama una vijimatatizo vya hapa na pale vya ngozi na unataka kuboresha ngozi yako basi jaribu kuogea sabuni ya liwa

NB: kama ukitumia liwa na ukiona inakuharibu ngozi badala ya kuipa afya acha kuitumia mara moja na umuone daktari

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...