Nov 27, 2012

sharo milionea afariki dunia...

Habari zilizoifikia blog ya cheyfitness hivi punde zinaripoti kwamba Msanii-Muigizaji wa filamu na mchekeshaji nchini maarufu kwa jina la "Sharo Milionea" amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea huko Lusanga, Muheza mkoani Tanga majira ya saa  2 usiku jana,

     Hussein Mkiety aka sharo milionea
 
Uongozi wa Blog ya cheyfitness unatoa pole kwa ndugu,jamaa, marafiki na watanzania wote kwa ujumla

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi....Amen.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...