Nov 29, 2012

MADHARA YA UTUMIAJI WA MIRUNGI (khat)

 
Matatizo na madhara ya Mirungi yaligunduliwa mwanzo katika mwaka 1935 na League Of Nations, Mwaka 1970 taasisi ya tiba ikaitenga madhara ya cathinone yanayopatikana katika Mirungi ambayo kikemikali inafanana na amphetamine, na hivyo katika mwaka 1971 ikaorodheshwa na United Nation kuwa ni miongoni mwa madawa ya kulevya.
 
mirungi

 
Utumiaji wa Mirungi husababisha madhara mbalimbali kiafya kama:
  1. Magonjwa ya vidonda vya tumbo (ulcers)
  2. Ukosefu wa haja kubwa (constipation)
  3. Utumiaji wa muda mrefu husababisha kuharibu utendaji kazi wa ini, na pia kusababisha ubadilikaji rangi meno, kudhoofika, na fizi kuuma na harufu ya mdomo
  4. Upungufu wa msukumo wa kufanya jimaa (sex drive). Na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu;
  5. Kupatwa na ugonjwa wa futuru/futuri/bawasiri/baasili – nyama inaoota kwenye utupu wa nyuma
  6. Upungufu wa usingizi
  7. Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo (Addiction)
  8. Walaji wengi huvuta na sigara, hata yule aliyekuwa havuti kabla ya kuanza kula Mirungi, hujikuta akizama kwenye uvutaji, na madhara huwa maradufu

 
mirungi
 
mirungi hujulikana pia kwa majina mbalimbali kama vile gomba, shamba, miraa, khat na kadhalika

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...