May 22, 2013

JISIKIE VIZURI NA JIONE MTANASHATI


 
kujisikia vyema kuhusu mwili wako ni jambo la msingi sana katika kujiona wewe ni bora.... ukijisikia vyema juu ya mwili wako lazima utautunza na kuwa mtanashati na pia na kujisikia vyema muda mwingi.

kujisikia vizuri kuhusu mwili wako hakuhitaji wewe kuwa mwembamba, unahitajika kuwa fit na mwenye afya njema na kujisikia vyema. vyovyote ulivyo wewe ni mzuri tatizo ni huo tunajisahau kujali afya zetu matokeo yake tunaangukia kwenye kula vyakula ambavyo vinatupelekea kwenye unene uliopitiliza ambao si mzuri kiafya.

hivyo basi vyovyote ulivyo jisikie vyema.... hakikisha unakula chakula bora na kufanya mazoezi mara kwa mara.

Apr 17, 2013

MADHARA YA VIATU VYA MCHUCHUMIO( high heels)



 
 
kwa miaka mingi viatu vya mchuchumio vimekua ni rafiki mkubwa wa wanawake na viatu hivi vina faida mbali mbali kama vile mwana mke kuonekana wa kileo, kuonekana mrefu, kuonekena una miguu mizuri na shepu nzuri....



 lakini pia viatu hivyo hivyo vya mchuchumio vina madhara makubwa kwa wavaaji ambayo yanaweza kuhatarisha afya ya mvaaji, madhara hayo ni kama:
- maumivu ya miguu
- kushindwa kutembea sawasawa
- maumivu ya mgongo
- sugu na vidole kwenda upande
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...