Jan 26, 2010

Lishe bora kwa afya

Lishe bora haimaanishi kufuata filosofia kali na za ajabu za lishe, kujikondesha kulikopitiliza au kujinyima kabisa kitu unachopenda, badala yake ni kujisikia vizuri, kuwa wenye nguvu na kuwa na afya.

Lishe bora ni ile inayosaidia kutunza na kuboresha afya, pia lishe bora ni muhimu kwa kuzuia maradhi mengi kama vile unene uliopindukia, magonjwa ya moyo, kisukari na kansa.


lishe bora inahusisha kula chakula chenye kukupatia kiasi sahihi cha virutubisho na maji, virutubisho vinapatikana katika vyakula vya aina mbalimbali.

Bette Calman - Bibi mtaalamu wa Yoga

Bette Calman ni bibi wa miaka 83 mwenye asili ya Australia ambaye ni ushahidi wa kuwa Yoga inaweza kufanya maajabu katika mwili wa binadamu. Watu ambao wana umri sawa na Bette wengi wao hawawezi hata kujisogeza lakini yeye bado anafundisha na kufanya yoga.



Bette bado ana uwezo wa kufaya Yoga katika 'positions'ngumu ambazo akifanya pamoja na vijana wanaweza kutia aibu.

TFF : Tiketi za kombe la Dunia zimeisha


Shirikisho la Soka Nchini (TFF) jana limesema tiketi zote 30 ambazo Tanzania imepewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa ajili ya mashabiki wa Tanzania kuona mechi ya Fainali za Kombe la Dunia itayofanyika Julai 11 nchini Afrika Kusini zimeshauzwa ambapo tiketi ya daraja la kwanza imeuzwa Dola 900ambazo ni sawa na Sh. Milioni 1.2

Afisa Habari wa TFF amesema kuwa tiketi kwa ajili ya hatua nyingine za mashindano hayo bado zipo nyingi za kutosha kwani kuna tiketi 60 kwa ajili ya mechi Na. 2 hadi Na. 48. Tiketi 30 za mechi ya ufunguzi ambayo itakuwa baina ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico kwenye Uwanja wa Soccer City mjini Johanesburg pia zimeshauzwa zote.

Jan 25, 2010

MAZOEZI YA VIUNGO


mazoezi ya viungo ni shughuli inayotakiwa kufanyika mara kwa mara ili kuboresha na kutunza ubora wa miili yetu. mazoezi ya viungo yanakuwezesha kufanya shughuli za kila siku kwa ufasaha na bila kupata uchovu uliopitiliza, pia mazoezi ya viungo yanasaidia kutufanya tukabiliane vyema na 'stress' za kila siku pamoja na kutupa wepesi katika matukio yanayohitaji uharaka wa kutenda.


ufanyaji wa mazoezi ya viungo mara kwa mara yanasaidia kutuepusha na maradhi ya mara kwa mara na kuwa na afya bora. Mazoezi yapo ya aina mbalimbali na kuna jinsi tofauti za kufanya mazoezi hayo kwa hiyo kila mtu anaweza kushiriki kwenye mazoezi kwa njia moja ama nyingine.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...