Jan 19, 2011

kufanya mazoezi kupita kiasi


kufanya mazoezi bila mpangilio kunaweza kukufanya uangukie kwenye kufanya mazoezi kupita kiasi jambo ambalo linaweza kukusababisha maumivu na pengine ugonjwa kabisaaa.
unawezaje kujua kama umefanya mazoezi kupita kiasi, hizi ni baadhi ya dalili za kufanya mazoezi kupita kiasi:
  • kizunguzungu cha mara kwa mara
  • maumivu ya misuli na viungo
  • kuchoka sana
  • mapigo ya moyo kwenda kasi uamkapo asubuhi
  • kusikia uvivu wa kufanya shughuli zako
  • kupoteza hamu ya kula

kama utaona dalili hizi na unafanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari wako ili kujua kama ni overtraining na hakuna athari zilizojitokeza kwa ajili ya overtraining hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...