Feb 7, 2010

TIBA YA LISHE KWA WAGONJWA WA ANEMIA


Hakuna tiba bora kama chakula na kila ugonjwa una chakula chake kama tiba. Mgonjwa hulazimika kutumia dawa za hospitali pale hali inapokuwa mbaya na ugonjwa unapokuwa umefikia hali mbaya.

Hata hivyo, baada ya mgonjwa kujijua ugonjwa unaomsumbua, hupaswa kujua pia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuacha kula, ili kudhibiti tatizo na hatimaye kuliondoa kabisa mwilini.

Leo tunaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula mgonjwa wa Anemia aina zote, ukiwemo Sickle Cell (magonjwa ya kupungukiwa damu mwilini kutokana na sababu mbalimbali).

APPLEST
ufaha au kama linavyojulikana na wengi ‘Apple’ ni tunda muhimu sana kwa wagonjwa wa Anemia. Wanaosumbuliwa na ugonjwa huu, wanashauriwa kula epo 2 hadi 3 kwa kila siku. Tunda hili linaelezwa kusaidia kuongeza kiwango cha madini ya chuma mwilini ambayo huhitajika sana kwenye damu.

VITAMIN B12
Ulaji wa Vitamin B12 ni muhimu sana kwa kinga na tiba ya ugonjwa wa Anemia. Chanzo kikuu cha vitamini hii ni vyakula vitokanavyo na wanyama, hasa nyama ya maini na figo. Nyama hii ni miongoni mwa tiba bora kabisa za ugonjwa huu.

KAHAWA NA CHAI
Hili ndiyo jambo la kuzingatia sana, kwani ndipo ambapo wagonjwa wengi hufanya makosa. Mgonjwa wa Anemia au Siki Seli hatakiwa kunywa chai wala kahawa kwa sababu vinywaji hivi huwa ni kikwazo kwa ufanyaji kazi wa madini ya chuma mwilini.Unapokuwa mgonjwa wa wa maradhi hayo na ukawa unakunywa chai na kahawa kama kawaida, huwezi kuudhibiti ugonjwa vizuri na dawa utakazokuwa ukitumia hazitafanyakazi ipasavyo, kwa sababu itakuwa ni sawa na mtu anayelala kwenye chandaru kilichotoboka.

BEETS ROOTS
Beets Roots ni aina fulani ya viazi ambavyo vinajulikana pia kama viazi pori. Viazi hivi ni muhimu sana kwa tiba ya ugonjwa wa Anemia kwani vina protini na madini mengi kama vile potassium, phosphorus, calcium, sulphur, iodine, iron, copper, carbohydrates, protein, fat, na vitamin B1, B2, B6, C na P. kwa sababu hii, beets ni tiba nzuri sana ya asili.

MAJI BARIDI
Aidha, uogaji wa maji baridi nao ni sehmu ya tiba asilia ya Anemia. Mgonjwa anashauriwa kuoga maji baridi mara mbili kwa siku. Aidha, uogaji huku ukiwa juani nao husaidia uzalishaji wa Red Cells ambazo ni kiungo muhimu cha damu.

ASALI NA LIMAU
Asali pia imetajwa kuwa tiba nzuri kwa wagonjwa wa Anemia. Changanya asali na limau kiasi kidogo na kunywa asubuhi kabla hujala kitu chochote. Hii nayo ni miongoni mwa tiba bora asilia za ugonjwa huu. Halikadhalika tende zimetajwa kutibu Anemia.

MASSAGE
Ufanyaji wa masaji kila siku nao ni muhimu kwa mgonjwa Anemia, kwani husaidia kuweka juu kiwango cha damu wakati wote. Hii nayo ni moja ya tiba rahisi kabisa unayoweza kuifanya nyumbani kwako.

MWISHO,
Mazoezi mepesi ya kila siku na yale mazoezi ya kuvuta na kushusha pumzi nayo ni muhimu na husadia sana katika kuweka damu katika hali inayotakiwa. Mgonjwa wa Anemia na siko seli akiishi kwa staili ya kufuata maelekezo haya, anaweza asisumbuliwe sana na ugonjwa huo kwa maisha yake yote.
NDUGU MDAU MAKALA HII NIMEITOA KATIKA BLOG YA http://abdallahmrisho.blogspot.com/ UNAWEZA KUPITIA HUKO KWA MAUTAMU ZAIDI KUHUSU MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA.

Feb 4, 2010

Kitambi "Beer Belly"

Mdau kama wewe ni mnywaji wa pombe unaweza kugundua kuwa tumbo lako limeanza kuwa kubwa au limeshakuwa kubwa kiasi cha kuning'inia. Kitambi ni tatizo linalotakea mara nyingi kwa wanaume pia hutokea kwa wanawake.

Jinsi nzuri ya kupunguza au kuondoa kabisa kitambini kupunguza kiasi cha Alcohol kinachoingia mwilini na kuanza kufanya mazoezi ya mara kwa mara. Beer ina kiwango cha juu sana cha calories ni ya pili ukiacha fat yenyewe.


Kama wazo la kuachana na kilevi linakuwia vigumu basi jaribu kutumia beer nyepesi ambayo ina kiwango cha chini cha calories ukilinganisha na beer ya kawaida.

Pia jaribu kupunguza kiwango chako cha unywaji, kunywa wakati wa weekend tu pamoja na kuwa na ulaji ulio na mpangilio na usisahau kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

Feb 3, 2010

Mji mpya yang'aa Winome Cup

Timu ya soka ya Kata ya Mji Mpya juzi ilianza vizuri michuano ya Winome Salama Cup baada ya kuifunga kata ya Uwanja wa Taifa mabao 4-1 katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

mji mpya ambayo ilionekana kujiamini na kuutawala mchezo huo, mabao yaliyowapa ushindi katika mechi hiyo yalifungwa na washambuliaji Juma Maboga na Keneth Emanuel ambao kila mmoja alifunga mabao mawili.

Unamkumbuka? SULEIMAN NYAMBUI

Suleimani Nyambui alizaliwa Februari 13, 1953, ni mkimbiaji mstaafu kutoka hapa Tanzania ambayealishinda:
  • Medali ya Shaba katika All-Africa Games mwaka 1978.
  • Medali ya Fedha katika mbio za mita 5,000katika Summer Olympics mwaka 1980.
  • Alishinda mara mbili Berlin Marathon mwaka 1987 na 1988.

Alihudhuria University of Texas at El Paso (UTEP) mwaka 1978-1982 ambapo alishinda mara nne 'titles' za NCAA (National Collegiate Athletic Association) kwenye mbio za mita 10,000 na mara tatu kwenye mita 5,000.

katika michezo ya Millrose iliyofanyika New York, Februari 1981 Nyambui alivunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 5,000 kwa kukimbia kwa dakika 13:20.4

Feb 2, 2010

" man boobs" ni matiti ya kweli?

Tom Cruise - hata mastaa nao wana boobs

Kitu kimoja ambacho wanaume hawakiombei na wanakilaani ni kuota matiti kama vile wanawake. hili ni jambo la kufedhehesha kwao lakini amini usiamini ni jambo la kawaida na linatokea kwa wanaume wengi.

Man boobs yapo ya aina tatu:
  • Gynecomastia - kwenye hii aina boobs zinakuwa za ukweli kabisaaa maana yake matiti hayo yanakuwa yamecontain breast tissue. aina hii ni ngumu kutoweka kwa mazoezi au lishe yanaweza kuondoka kwa kufanyiwa upasuaji au dawa maalumu.
  • Pseudogynecomastia - hapa ni matiti yaliyo jaa mafuta pengine kwa sababu ya ulaji mbaya au uvivu wa mazoezi. haya si matiti ya kweli na yanaweza kukabiliwa na mazoezi na lishe bora.

  • aina ya tatu na ambayo inatokea kwa wanaume wengi ni ya matiti yaliyo na mchanganyiko wa breast tissue na mafuta. matibabu ya asili (mazoezi na lishe bora) kwa watu wenye aina hii ya matiti yanategemea mtu na mtu.


Simba SC yaichapa Toto


Simba jana iliendelea kudhihirisha ubabe wake katika ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Toto Africa ya hapa mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mjini Mwanza.

Mussa Hassan 'Mgosi' ndiye aliyepachika bao la kwanza katika dakika ya 52 na dakika mbili baadaye Ramadhani Chombo 'Redondo' aliimaliza Toto baada ya kupachika bao la pili.

katika mechi ya jana kulikuwa na imani za kishirikina ambapo Simba walidai kukuta chumba choa kimemwagiwa vitu vya majimaji vyekundu vinavyofanana na damu, hali iliyomlazimu Katibu Mkuu wa Simba Kaduguda kumuandikia barua Kamisaa wa mchezo huo kwamba hawatatumia chumba chao kutokana na tukio hilo.

Feb 1, 2010

Umesikia? Udaku ni mzuri kwa afya!!

udaku unasambaa kwa haraka sana..amefanya nini?...anatoka nae? na ni watu wachache sana wenye uwezo wa kuziba masikio kuacha udaku upite.



Gazeti la Hormones and Behavior la Marekani limeandika kuwa wachunguzi wa mambo wametupilia mbali hoja kuja udaku ni kisauti tu kinachopita nyuma ya sikio kisicho na maana yoyote badala yake wanashauri kuwa udaku uwe ni moja ya mambo ya msingi ya kufanyiwa uchunguzi linapokuja suala la makundi ya jamii.

udaku si mzuri tu kwa sababu unaweka watu pamoja lakini pia unasaidia kusambaza habari za msingi kuhusu tabia za watu ambazo huwa haziwekwi kwenye CV za watu.




Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...