Dec 7, 2010

JISIKIE VIZURI JINSI ULIVYO........


Kila mtu, mnene au mwembamba alishawahi kwa kipindi fulani kujifeel negatively kuhusu miili yao. Njia rahisi ya kujisikia vizuri kuhusu mwili wako ni kuhakikisha kwamba unakuwa mtanashati kwa kiwango cha juu unachoweza. sio unatoka wako umesahau kunawa uso, umesahau kupiga pasi nk.


Mambo ya kuzingatia:
1. Unatakiwa kujiambia kila siku unapojitazama kwenye kioo kuwa hicho unachoona ni kizuri na utaendelea kukiboresha. hakikisha umependeza, unanukia vizuri kama ni mwanaume kaka una bashasha na bibie full mashamsham hapo toka elekea kwenye shughuli zako hakika utakuwa unajisikia vizuri.

2. Rome haikujengwa kwa siku moja!! kama una kilo 101 ukipunguza nusu jisifie ona hayo ni mafanikio sio una kilo 101 unataka ulale uamke ufanane na shoga yako mwenye kilo 51. jipongeze kwa kila hatua ndogo unayo piga na usikate tamaa.

3. Hakikisha unakula mlo sahihi unaoendana na matakwa yako, kama unataka kupunguza uzito basi hakikisha unakula mlo sahihi.


4. Kujiremba.
-Hakikisha unapotoka kwako asubuhi umejiremba, usoni namaanisha.

-Hakikisha nyele zako ziko vizuri, tafuta mionekano mipya ya nywele, jaribu style mpya za nyele sio unatutokea kwako na  mibutu au minywele imeota kama saluni huzioni vile.

-Vaa nguo inayoendena na rangi yako na mwili wako sio ujipige mimake-up ya ukweli,nywele unaeleweka halafu nguo unatuvalia
 mazwazwa...piga pamba unayokufanya utoke.

 -Vaa viatu vinavyokufanya uonekane smart.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...