Mar 1, 2010

jamani hii ni hatari...!!

mdau wa blog hii Catherine Salim aliyepo China amenifowardia hii email ili niipublish kwa faida ya wadau wote wa blog hii:

HAKUNA KUPONA
Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa kitabibu, baadhi ya kuku wa kufugwa wanaoingia sokoni wamekuzwa kwa kutumia ‘utundu’ wenye hatari wa baadhi ya wafugaji wasio waaminifu kwa kulisha mifugo hiyo dawa za ARV ambazo huwafanya kuku hao kuonekana wakubwa na wanene kwa muda mfupi.


Uchunguzi huo unakwenda mbele zaidi na kubainisha kwamba, tabia za dawa hizo ambazo ni kujenga mwili na kuimarisha kinga ya magonjwa kwa mwathirika wa Virusi vya Ukimwi, ndiyo inayompata mlaji wa kuku hao.

Inadaiwa kuwa, kuku hao wanapokula chakula kilichochanganywa na dawa hizo, huweza kutumia siku kumi na mbili hadi kumi na nne kutoka kuwa vifaranga hadi utayari wa kuingizwa kwenye soko la walaji.


Kwa mujibu wa kijana mmoja ‘profesheno’ wa kutunza kuku katika moja ya nyumba maarufu kwa uzalishaji,  alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini alibainisha kuwa hajui bosi wake anapochukulia vidonge hivyo vya ARV’S.



MADHARA:
Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbi ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, mtu anayependa kula kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV na yeye huanza kunenepa kupita kawaida, lakini uzito unaweza kuwa tofauti na unene ‘boya’.


Mtabibu huyo aliongeza kuwa, watoto wengi wanaozaliwa siku hizo ambao wazazi wao wamekuwa watumiaji wazuri wa kuku, hukua haraka kiasi kwamba, mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27.


Aidha, alidai kuwa, wengi ambao kuku hao wamekuwa chakula chao kikuu, hufika mahali wanakuwa ‘legelege’ katika utendaji wa kazi wa kila siku tofauti na zamani huku sehemu kubwa ya chakula hicho ikiangamiza ‘pati’ ya subira na uvumilivu na mlaji kuwa na hasira.


Dalili nyingine ni mtu kuhisi muda wake wa kuchoka unakuwa mfupi akilinganisha na zamani na wakati mwingine hali ya kuhisi kusinzia humtawala hata kama anafanya kazi.

 



ONYO:
Onyo la kwanza lilitolewa na Daktari huyo kwa wafugaji wasiokuwa waaminifu, kuachana na tabia hiyo mara moja kwani wanaharibu nguvu kazi ya kesho itakayowarudi wao wenyewe, kwani wapo walaji ambao ni ndugu, jamaa au marafiki zao.


Wakakumbushwa kuwa, mwisho itafika mahali taifa litakuwa na watu wenye uwezo mdogo wa kufanya kazi na hivyo taifa kuangamia kwa umaskini au kubobea kwa kuwa ombaomba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...