Mar 4, 2010

watu watatu wapatwa na mafua ya nguruwe buzwagi

*Wagonjwa watatu wathibitishwa kuwa na virusi vya H1N1

*Hali imethibitiwa,
*Wataalamu wamepelekwa na dawa zimeshafikishwa eneo husika
*Karantini imewekwa bila kudhuru uzalishaji


Machi 3, 2010, Kahama, Shinyanga –
Mgodi wa Buzwagi jana ulithibitisha kuwepo kwa wagonjwa watatu ambao ni wafanyakazi wa mgodi wenye virusi vya H1N1, au mafua ya nguruwe. Wafanyakazi hao ni wakazi wa mgodini na mpaka sasa hali zao ni nzuri na wanaendelea kupata nafuu.


Hapo awali mgodi ulikwishachukua hatua za dharura, ambazo ni pamoja na; kupima afya za wafanyakazi , kuwatenga walioathirika na kuwapatia dawa za Tamilflu ambazo ni maalum kwa kutibu virusi hivyo.


Mgodi huo ulituma vipimo vinne kwa ajili ya upambanuzi wa aina ya virusi, katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Maswala ya Utabibu (NIMRI), ilioko Dar es Salaam. Hapo Jumaatatu Machi 1, NIMRI ilirudisha majibu yaliothibitisha uwepo wa virusi vya H1N1 kwenye vipimo vitatu kati ya vinne vilivyowasilishwa.


Mgodi wa Buzwagi unafanya kazi kwa karibu na daktari wa wilaya ya Kahama pamoja na Wizara ya Afya kufuatilia hali ya walioathirika na kuthibiti kusambaa zaidi kwa ugonjwa. Vilevile timu ya wataalamu imetumwa kutoka Wizara ya Afya na bingwa wa maswala ya afya wa Barrick pia yupo mgodini kutoa ushauri na kusimamia matibabu.


Wafanyakazi wote wasio na majukumu ya lazima wamerudishwa majumbani na mienendo ya watu wanoingia na kutoka mgodini unathibitiwa ipasavyo.



Mpaka sasa watu 21 wako kwenye karantini na wanapatiwa matibabu kamili. Bado ni mapema mno kubaini chanzo cha virusi kwa vile uchunguzi bado unaendelea.


habari hii ni kwa hisani ya http://issamichuzi.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...